SUMU

Advertisements

Sumu hino ina siri, inapaswa uelewe

Advertisements

Siku zote ukariri, na inate kwenye ndewe

Jifunze kuwa mahiri, anza sasa sichelewe

Nisemayo ni ya kweli, sumu ni mimi na wewe

 

Sumu ni yule rafiki, anauma kipuliza

We hujui ni nafiki, urafiki kapagaza

Yuyo huyo ni ashiki, shida zako kutangaza

Nisemayo ni ya kweli, sumu ni mimi na wewe

 

Sumu ni wangu mapenzi, nimpendaye kwa upana

Kaniteka kumuenzi, namsahau Rabana

Ananitungisha tenzi, hata zisizo za maana

Nisemayo ni ya kweli, sumu ni mimi na wewe

 

Sumu ni kaka na dada, wanotupa tabasamu

Kumbe kwao ni ibada, kutuchamba kwa hatamu

Wamehitimu na shahada, za fitina aalimu

Nisemayo ni ya kweli, sumu ni mimi na wewe

 

Sumu ni mimi na wewe, mtunzi na msomaji

Leo hii usifiwe, kesho umwaiwe maji

Kwa hili nilaumiwe, kwa lile nivishwe taji

Nisemayo ni ya kweli, sumu ni mimi na wewe

 

©Ustadh Andayi

Malenga asokufa

#IpoSiku

#HeriYaja

<script data-ad-client=”ca-pub-4344699775575136″ async src=”https://pagead2.googlesyndication.com/pagead/js/adsbygoogle.js”></script>

Advertisements

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *