NYUMBANI KWEMA AFRIKA

AdvertisementsYangu nudhumu natunga,mengi kuwaelezeni,
Tungo hili kuanganga, uborawe fahamuni,
Hakika sita’bananga, kuusoma mudhikeni,
Nyumbani kwema Afrika, katu tusiidhalili.

AdvertisementsYetu mazingira ali, mvuto kwa watalii,
Tuwe’nye bora adili, mandhari kulindenii,
Itakuwa afadhali, misitu kutunzanii,
Nyumbani kwema Afrika, katu tusiidhalili.


Hadhi yetu tulindeni, kwa ubora wetu wasomi,
Ndege tusiabirini, kwetu tuwe wabaghami,
Hali ya akademini, tuboresbe wetu usomi,
Nyumbani kwema Afrika, katu tusiidhalili.Ajira kuitafuta, Ulaya tusi’lekee,
Zao mila kufuata,majuto tusabishie,
Tujitenge na ujeta,nasi tujitegemee,
Nyumbani kwema Afrika, katu tusiidhalili.Tamaduni za ugeni, zake athari ni chungu,
Moja kiwa mavazini, yaletwayo na wazungu,
Mila aula twamini, zipendwazo naye Mungu,
Nyumbani kwema Afrika, katu tusiidhalili.‘zidishe utangamano, katika yetu maisha,
Tubadilishe maono, uchumi kuamirisha,
Tuondowe farakano, barani kusitawisha,
Nyumbani kwema Afrika, katu tusiidhalili.Twangaze Elimu yetu, barani kuleta mwanga,
Yao haki wanawetu, kwao kwondoa ubunga,
Tuuzibe utukutu, ubahaluli kupinga,
Nyumbani kwema Afrika, katu tusiidhalili.Barabara kuzijenga, wetu wandisi wajuzi,
Wasomi wetu si ‘bunga, katu hawana upuzi,
Mbona wafanywe wachanga, wenye sufufu ajizi,
Nyumbani kwema Afrika, katu tusiidhalili.Zetu lugha tujivune,kuzilinda tamaduni,
Hata usiku manane, ziweze kutumikani,
Tusihisie mavune,kwenye yetu ma’ngezini,
Nyumbani kwema Afrika, katu tusiidhalili.

Viongozi twadhibike, zetu ahadi timize
Tusiwe wenye makeke, timiza agano ziweze
Tusisababishe shake, kwetu mwanga siangaze
Nyumbani kwema Afrika, katu tusiidhalili.Kando kalamu naweka, wangu ujumbe mepasha,
Tuwe nao mualaka, bara nzima taboresha,
Tuzidishe kuauka, zote ‘dara kwamirisha,
Nyumbani kwema Afrika, katu tusiidhalili.


©Vincentokwetso
2021 Poetry

Mtunzi: VINCENT OKWETSO
Mugema wa Manudhumu.

Advertisements

One Reply to “NYUMBANI KWEMA AFRIKA”

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *