MUDA WANGU UMEWADIA

AdvertisementsKwa utunzi mimi sio guru,
Ila nimeona ujumbe huu utaniweka huru,
Ni dhahiri kuwa sihitaji kuishi tena,
Kaburini mimi naelekea..

AdvertisementsSamahani kwa kuboronga lugha,
Ni kutafuta natafuta uga,
Angalau pointi nusu nitakapozikwa,
Nahisi maishi yangu humu duniani kafika tamati..Usishangae lugha yangu mbaya,
Ni hisia kutoka moyoni natoa sina ubaya,
Kiwango cha elimu sijafika majuu,
Ila bora ujumbe umewafika..Babangu mzazi sijawai mwona,
Na pia sitarajii kumwona tena,
Sababu muda umeshaa wadia,
Muda wangu mimi kuondoka duniani..

Mamangu sasa hivi yupo kwa ndoa ya tatu,
Simpi lawama maanake kanishughulikia hadi kidato cha tatu,
Naelewa ni pendo lake anatafuta,
Singependa kumzidisha mzigo,
Ni heri niondeke apunguze mawazo..

Kila kuchao najitahidi kuwa bora,
Ila kichwa changu kimejaa maumivu ya hora,
Baada ya “MRI” daktari alisema mi mzima,
Ni uzembe nasingizia kichwa..


Babu yangu tunayeishi naye aliyasikiza yote hayo,
Kisha kaniambia ni kazi nitafanya kutumia wayo,
Kila asubuhi yupo mlangoni kuniamsha nitoke na ng’ombe,
Jioni nirudi nao wakiwa wameshiba ndio nipate tonge la chakula..Kichwa kilipokosa kuhurumiwa mgongo haukusita,
Kifua nacho, shingo, sasa hivi nina magonjwa sita,
Ni kweli Mola aniita mbinguni nikapumzike,
Muda umewadia wenzangu kwaherini..


Japo sina hata wa kuaga shairi nimebuni,
Wote walinihepa sababu ya hali yangu duni,
Natumahi nitapata hali njema mbinguni,
Wakifikishie ujumbe muda wangu ulikua umewadia.©Asilikwabrian2021
Mwandishi:
~Asilikwa Brian
Nambari:+254758034781

Advertisements

4 Replies to “MUDA WANGU UMEWADIA”

  1. Also visit Wanda Poetry Hub facebook page I published it there,just to support a friend. Good work you are doing

    © Wanda’s Ink Pen
    ®Wanda The Poet ✍️
    #The Hand of God

  2. Pingback: Wanda's Ink Pen

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *